Kuelekea 2025 Lissu: CHADEMA ikiondoka kwenye misingi iliyonifanya nijiunge nacho, nitaondoka. CHADEMA siyo mama yangu wala dini yangu
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA- Bara, Tundu Lissu amsema iwacha CHADEMA itaacha misingi yake ailiyomfanya ajiunge na chama hicho basi ataondoka katika chama hicho na sio dhambi kufanya kuvyo kwani Chama cha Siasa sio mama yake wa dini yake
Akizungumza kupitia Mtandao wa Clubhouse amesema "Mwalimu Nyerere katika mojawapo ya kauli zake nyingi aliwahi kusema kwamba CCM siyo mama yangu na ikiacha misingi yake nitaiacha, ilikuwa kauli ya Mwalimu kuhusu chama alichokianzisha, kwa hiyo unataka mimi niseme kwa mazingira yoyote yale vyovyote itakavyokuwa sitahama CHADEMA? ni mama yangu?"
Ameongeza "Niliingia CHADEMA miaka 20 iliyopita na nimekuwa hapa miaka yote hii na Mungu anirehemu niendelee kuwa CHADEMA wakati nayo ikiendelea kuishi, lakini CHADEMA siyo dini na siyo mama yangu, ni chama cha siasa kikiondoka kwenye misingi yake iliyonipeleka nikajiunga nacho nitaondoka, nitakuwa sina sababu ya kubaki na hiyo siyo dhambi kwa sababu siyo dini na siyo mama yangu nikitumia maneno ya Mwalimu, ni chama cha siasa, vyama vya siasa huja na kuondoka, sisi binadamu tunakuja na kuondoka"
No comments:
Post a Comment