INEC YAENDESHA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 10 August 2024

INEC YAENDESHA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA SHINYANGA

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Mratibu wa Uandikishaji Mkoa wa Shinyanga, Maafisa waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga leo Jumamosi Agosti 10,2024

NA NEEMA NKUMBI- HUHESO DIGITAL SHINYANGA

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mheshimiwa Jaji (R) (MST) Mbarouk Salim Mbarouk leo agosti 10, 2024 amefungua mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Mkoa wa Shinyanga.

Jaji Mbarouk amesema washiriki wa mafunzo hayo muhimu ni pamoja na Mratibu wa Uandikishaji wa Mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri.

Pia amewapongeza washiriki wote kwa kuteuliwa na Tume kuendesha na kusimamia zoezi la uboresha wa daftari la kudumu la wapiga kura.

" sina shaka kuwa kuteuliwa kwenu kunatokana na ujuzi, uwezo na weledi mlionao katika kutekeleza majukumu ya kitaifa likiwemo zoezi la uboreshaji wa daftari ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025", amesema Jaji Mbarouk.

"Mafunzo haya yatahusisha namna ya ujazaji wa fomu pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura( Voters Registration System-VRS) ili muweza kupata uelewa wa pamoja utakaowapa fursa ya kutumia kwa ufasaha mfumo huo pamoja na vifaa vingine vya kuandikisha wapiga kura", amesema Jaji Mbarouk.

"Aidha, Maafisa TEHAMA watapatiwa mafunzo maalum ya jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiufundi( troubleshooting) endapo zitajitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura vituoni",ameongeza Jaji Mbarouk.

"Pia Tume imetoa kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uboreshaji wa Daftari kwa asasi za kiraia 157 na asasi za kiraia 33 kwa ajili ya uangalizi wa zoezi hilo hivyo ni muhimu kutoa ushirikiano kwa asasi hizo zitakapofika kwenye maeneo yenu kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao, Tume itawapa vitambulisho kwa urahisi wa kuwatambua",amefafanua Jaji Mbarouk.

Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura linatarajiwa kufanyika tarehe 21- 27/8/2024 mkoani Shinyanga.

Wapiga kura wapya wanaotarajiwa kuandikishwa katika Mkoa wa Shinyanga ni 209,951 na waliopo katika daftari la kudumu la wapiga kura ni 995,918, hivyo tume inatarajia baada ya uandikishaji Mkoa wa Shinyanga utakuwa na wapiga kura 1,205,869.

Vituo 40,126 vya kuandikisha wapiga kura vitatumika katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2024 ambapo kwa Mkoa wa Shinyanga kuna vituo 1,339 vitakavyotumika kwenye uboreshaji kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeko la vituo 122 katika vituo 1,217 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20

Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifungua mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Mratibu wa Uandikishaji Mkoa wa Shinyanga, Maafisa waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga

Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile akizungumza wakati wa mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Uchaguzi

Hakimu Mkazi, Mhe. Goodselda Charles Kalumuna akielezea kuhusu kiapo cha kutunza siri na tamko la kujitoa uanachama au kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa kwa Mratibu wa Uandikishaji Mkoa wa Shinyanga, Maafisa waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga.
Mratibu wa Uandikishaji Mkoa wa Shinyanga, Maafisa waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga wakila kiapo cha kutunza siri na tamko la kujitoa uanachama au kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa wakati wa kutekeleza majukumu yao 
Mratibu wa Uandikishaji Mkoa wa Shinyanga, Maafisa waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga wakila kiapo cha kutunza siri na tamko la kujitoa uanachama au kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa wakati wa kutekelema majukumu yao
Mratibu wa Uandikishaji Mkoa wa Shinyanga, Maafisa waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga wakila kiapo cha kutunza siri na tamko la kujitoa uanachama au kutokuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa wakati wa kutekeleza majukumu yao
Maafisa waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mafunzo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso