EXIM BENKI YAKABIDHI VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA MILION 25 KATIKA HOSPITALI YA MANISPAA YA KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 29 August 2024

EXIM BENKI YAKABIDHI VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA MILION 25 KATIKA HOSPITALI YA MANISPAA YA KAHAMA

Mkuu wa Wilaya Mboni Mhita akipokea vifaa tiba vilivyotolewa katika hospitali ya Manispaa ya Kahama

NA NEEMA NKUMBI - HUHESO DIGITAL KAHAMA

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita ameipongeza Exim benki kwa kutoa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni ishirini na tano katika hospitali ya Manispaa ya kahama.


Mboni amesema hayo agosti 29 wakati wa makabidhino ya vifaa tiba hivyo yaliyofanyika katika hospitali ya Manispaa ambapo amesema vifaa hivyo vimekuja wakati mwafakwa na vitasaidia wahudumu wa afya kuhudumia wagonjwa kwa wakati.


Mkuu wa masoko na mawasiliano wa Exim benki Tanzania Stanley Kafu akitoa hutuba wakati wa kukabidhi vifaa tiba kwa hospitali ya Kahama amesema dhamira ya benki yao ni kusaidia jamii na kuchangia maendeleo ya sekta ya afya nchini.


"Benki yetu imekuwa karibu na jamiiinayotuzunguka na kupitia mpango wetu wa kurudisha kwa jamii unaojulikana kama exim cares, tumekuwa tukishiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo na kijamii katika sekta kadhaa nchini kama vile mazingira, elimu, uwekezaji wa kiuchumi, ubunifu na leo tuko hapa kwa ajili ya jambo muhimu la afya", amesema Stanley


Stanley amesema kufunguliwa kwa tawi lao kahama litaleta maendeleo kwani wanatoa huduma bora za kibenki zenye ubunifu na umakini, pia kusukuma gurudumu la maendeleo.


"Tunatambua na kuipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia ilivyojikita katika kukabiliana na changamoto katika sekta ya afya, ikiwemo uhaba wa vifaa tiba, upungufu wa vitanda, madawa na uchache wa watoa huduma, sisi tumetambua jitihada hizi na tumejitolea kuunga mkono serikali yetu kwa kutoa vifaa tiba", amesema Stanley.


Aidha Mganga Mkuu wa hospitali ya Manispaa ya Kahama Dr Baraka Msumi ameipongeza Exim benki kwa msaada wao na ameahidi kuvitunza vifaa hivyo ili viendelee kuwasaidia wagonjwa katika hospitali hiyo.


Pia mjumbe wa kamati ya usimamizi wa hospitali ya kahama Bernad Mapalala amesema vifaa hivi vitasaidia kupata huduma iliyobora.
Mkuu wa Wilaya Mboni Mhita akipokea vifaa tiba vilivyotolewa katika hospitali ya Manispaa ya Kahama
jengo la hospitali ya Manispaa ya Kahama
Vifaa tiba vilivyotolewa na benki ya Exim katika hospitali ya Manispaa ya kahama
Baadhi ya wafanyakazi wa Exim benki waliokuwepo katika  tukio la kukabidhi vifaa tiba

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso