YUSUF MANJI AFARIKI DUNIA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 1 July 2024

YUSUF MANJI AFARIKI DUNIA



Yusuf Manji enzi za uhai wake
​Mfanyabiashara maarufu na aliyekuwa mdhamini wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amefariki dunia Jumamosi Juni 29, 2024 saa 6 usiku katika Jimbo la Florida nchini Marekani alipokuwa anapatiwa matibabu.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na mtoto wake, Mehbub Manji akizungumza na Mwananchi Digital muda mfupi uliopita.

Yusuf Manji alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Quality Group Limited (QGL), kampuni inayojihusisha na sekta mbalimbali kama vile magari, ujenzi, vifaa vya kilimo, utalii, huduma za afya, na mali isiyohamishika.

Manji pia alifahamika kwa kujihusisha na shughuli za kijamii na misaada mbalimbali nchini Tanzania. Pia amewahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga.

Pia Manji alijihusisha na siasa kupitia Chama cha Mapinduzi na kufanikiwa kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu Manispaa ya Temeke. Septemba 6, 2017 alipoteza sifa ya Udiwani kutokana na kutohudhuria vikao zaidi ya sita na vikao vya kamati vya maendeleo ya halmashauri ya Temeke zaidi ya vitatu.

Atakumbukwa kwa mafanikio makubwa na mchango wake katika uchumi wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso