WAZIRI MKUU AZINDUA HOSPITALI YA RUFAA YA TOSAMAGANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 6 July 2024

WAZIRI MKUU AZINDUA HOSPITALI YA RUFAA YA TOSAMAGANGA



*_Azipongeza taasisi za dini kwa kuendelea kutoa huduma za kijamii_*


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezipongeza taasisi za dini likiwemo Kanisa Katoliki kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi.


Amesema kuwa kitendo cha Kanisa Katoliki cha kuamua kuipandisha hadhi Hospitali ya Tosamaganga na kuwa Hospitali ya Rufaa kwa ngazi ya Mkoa ni cha kishujaa kwani kitaufaanya mkoa wa Iringa kuwa na hospitali mbili za rufaa na hatimaye kupunguza adha kwa wakazi wa mkoa huo kusafiri kwenda mikoa ya Dar es Salaam na Dodoma kufuata huduma za kibingwa.


Ametoa pongezi hizo leo (Jumamosi, Julai 06, 2024) mara baada ya kuzindua hospitali ya rufaa ya Tosamaganga ngazi ya Mkoa pamoja na huduma za mionzi kwenye hospitali hiyo, iliyopo wilayani Iringa, mkoani Iringa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso