WAZIRI MKUU ATOA WITO KWA TAASISI ZA DINI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 19 July 2024

WAZIRI MKUU ATOA WITO KWA TAASISI ZA DINI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa taasisi zote za dini nchini kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutoa mchango kwenye maendeleo ya taifa.




Amesema kuwa taasisi za dini zina uwezo mkubwa wa kutoa huduma imara za kiroho na kugusa maisha ya watu katika jamii na kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kisiasa.


Ametoa wito huo leo (Ijumaa, Julai 19, 2024) kwenye Kilele cha Mkutano wa Baraza la Maaskofu wa Makanisa ya Pentekoste Tanzania (CPCT), uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Biblia Miyuji jijini Dodoma.


“Tuna kila sababu ya kuyashukuru Makanisa kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuleta maendeleo ya wananchi kwa ujumla, yamekuwa sehemu ya suluhisho katika changamoto za kijamii kama vile umaskini, elimu duni, na matatizo ya kiafya”


“Nitumie fursa hii kusisitiza taasisi za dini kuendelea kuimarisha ushirikiano na Serikali na kuendelea kuiishi kwa vitendo kaulimbiu yenu ya Palipo na Umoja, Bwana huamuru baraka! Bwana huamuru baraka, palipo na Umoja”


Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inathamini uwepo na mchango wa taasisi za dini katika kuhubiri amani na utulivu nchini “Siri ni ya haya yote ni sababu ya uwepo wa dini katika kuhubiri maadili, mshikamano, upendo uvumilivu na kuwa wamoja, Serikali pekee tusingeweza”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso