Mamlaka za afya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimesema takriban watu tisa wamefariki kufuatia msongamano uliokumba tamasha lililohudhuriwa na watu wengi kupita kiasi.
Tamasha hilo la mwanamuziki wa nyimbo za Injili Mike Galambay lilikuwa likifanyika katika uwanja wa Martyr katika mji mkuu, Kinshasa, Jumamosi.
Kulingana na vyombo vya habari nchini humo, watoto kadhaa
wanaripotiwa kuwa miongoni mwa watu waliofariki, huku watu wengine wakilazwa
katika wodi za wagonjwa mahututi baada ya ajali hiyo.
Gavana wa Kinshasa, Daniel Bumba, ametoa taarifa kulaumu kitendo
cha kuwepo kwa watu wengi kupita kiasi.
Waandaaji wa tamasha hilo, Maajabu Gospel, wamesema maafisa wa
usalama walijaribu kuwatuliza watu waliokuwa wanaleta vurugu, kitendo ambacho
kimesababisha watu kupoteza maisha yao.
Waandaji wameeleza
kuwa uwanja wa Martyr, ambao unachukua watu 80,000,
ulikuwa na watu 30,000 katika tanasha hilo lililofanyika siku ya Jumamosi.
Tukio kama hili lilitokea mwaka 2022 kwenye tamasha la mwanamuziki
Fally Ipupa ambapo watu 11 walipoteza maisha.
No comments:
Post a Comment