mgeni rasmi kulia pamoja na mkurugenzi wa manara foundation kulia wakikabidhi mahitaji ya shule kwa watoto wa New Hope Ophan Center
NA NEEMA NKUMBI HUHESO FM - KAHAMA
Mkurugenzi wa Manala Foundation Mhandisi Manala Tabu Mbumba akisoma risala wakati wa uzinduzi wa foundation yake
Watoto arobaini kutoka kituo cha kulelea Watoto yatima na wasiojiweza New Hope Ophan Center kilichopo mtaa wa Mwime ya Makungu kata ya Mwendakulima wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga wamepokea mahitaji mbalimbali kama sare za shule kwa Watoto wakike na wakiume pea 40, madaftari katoni 2,kalamu za wino katoni 10,kalamu ya mkaa katoni 10, miswaki,kiwi mafutaya kupaka,rula dazani 10 pamoja na vifutio dazani 10.
Msaada huo umetolewa na Mkurugenzi wa Manala Foundation Mhandisi Manala Tabu Mbumba wakati wa uzinduzi wa tawi laTaasisi hiyo Wilayani Kahama lenye makao makuu Dar es salam amesema wanatambua changamoto zinazowakabili jamii kama ukosefu wa makazi, elimu duni pamoja na huduma za afya zisisotosheleza.
Akisoma risala Mkurugenzi wa Manara foundation wakati wa uzinduzi amesema lengo la foundation yake ni kusaidia kutoa elimu iliyobora kwa kumwezeshakila mwenye sifa kupata elimu bila ubaguzi, kuboresha ufikiaji wa huduma za afya kwani hakuna maendeleo pasipokuwa na afya iliyobota , kuwezesha ukuaji wa Uchumi kwa kuwawezesha wajasiriamali pamoja na kukuza uhifadhi wa mazingira.
Kwa upande wake Mgeni rasmi Mgeni Rasmi ni Jusper Charles Kujicha Mshauri wa Biashara kutoka shirika Binafsi amewaasa wananchi wa Kahama kuitumia Manara Fondation kwa kushirikiana nao ili msaada unaotolewa uwe na manufaa pia ameongeza kuwa atato ushirikiano katika kutatua changamoto.
Akitoa shukurani kwa niaba ya Watoto hao Victor Boshegi amesema anaipongeza sana Manara Foundation inayojihusisha na kutoa misaada mbalimabali kwa Watoto yatima na wasiojiweza kwa kuwapatia Mahitaji hayo yatakayowasaidia Watoto kwenda shule bila shida.
Mwakilishi wa kituo cha kulelea watoto yatima Victor Boshegi akitoa pongezi kwa taasisi ya manara foundation baada ya kupokea msaada
baadhi ya watoto waliopewa msaada wakicheza mziki
No comments:
Post a Comment