WANANCHI WA NAMICHINGA WAISHKURU SERIKALI KWA KUJENGEWA KITUO CHA AFYA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 15 July 2024

WANANCHI WA NAMICHINGA WAISHKURU SERIKALI KWA KUJENGEWA KITUO CHA AFYA



Wananchi wa Kata ya Namichinga Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi wameishukru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujenga kituo cha Afya ambacho kitahudumia wananchi waliokuwa wakitembea zaidi ya kilomita 16 hadi 20 kufuata huduma Ruangwa Mjinina maeneo ya jirani.


Wananchi hao akiwemo Julian Futali na Mussa Makamuyanga wakizungumza mbele ya Mkurugenzi wa Afya,Ustawi wa Jamii na LIshe Ofisi ya Rais - TAMISEMI alipotembelea kituo hicho na kukagua maendeleo ya ujenzi na mazingira ya utoaji wa huduma akiwa ameambatana na Timu kutoka Ofisi ya Rais - TAMISEMI wamesema kina mama wajawazito na wagojwa wengine walikuwz wanapoteza maisha kutokana na umbali hivyo uwepo wa kituo hicho unakwenda kuokoa kundi kubwa la wananchi waliokuwa wakitembea umbali mrefu na gharama kubwa kufuata huduma za Afya.




Akizungumza kwa niaba ya katibu mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI,Mkurugenzi wa Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais - TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amewambia wananchi hao kuwa kituo hicho kitaanza kutoa huduma rasmi tarehe 01,Agosti 2024.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso