WACHIMBAJI WALALAMIKIA UKOSEFU WA HUDUMA YA CHOO MGODINI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 4 July 2024

WACHIMBAJI WALALAMIKIA UKOSEFU WA HUDUMA YA CHOO MGODINI





Afisa madini mkazi Mkoa wa kimadini Kahama Eng Joseph Kumburu akitoa agizo kwa uongozi wa mgodi wa nyikoboko akiwataka kupanga maeneo pamoja na usafi wa mazingira

NA NEEMA NKUMBI HUHESO DIGITAL - KAHAMA


Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu waliopo mgodi wa Nyikoboko Halmashauri ya Msalala Mkoa Shinyanga wamelalamikia ukosefu wa huduma ya choo katika mgodi huo ambao umeanzishwa wiki tatu zilizopita.


Mchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu Maganga Emanuel
ameeleza kuwa hali ya mgodi huo ni mbaya kwani hakuna choo wanajisaidia popote hali inayohatarisha afya zao.


" hali ya mgodi ni mbaya maana hakuna choo tunajisaidia mahali popote ambapo nitaona hapa nitajisitiri hili hii inatishia afya zetu kwa sababu huwezi kufanya kazi kama hauna afya nzuri", alisema Magaga .

Mfanyabiashara wa chakula katika mgodi huo Rehema Hasan ameuomba uongozi wa mgodi kuwajengea choo ili waweze kuendelea kufanya biashara zao maana yakitokea magonjwa ya mlipuko watafukuzwa.


Kwa upande wa ulinzi na usalama wa mgodi huo Anold Benedicto amesema wamejipanga kuhakikisha watu wanaoingia katika mgodi huo wanakuwa salama.


Katibu wa kamati ya ulinzi wa mgodi huo Sikujua Edward amesema wamejipanga kukabiliana dhidi ya ukatili kwa wanawake katika eneo la mgodi kwani wanawake wanaonewa kwa kudhurumiwa na kubakwa pia wanazuia watoto wadogo kuingia mgodi.


Aidha Meneja wa Mgodi huo Charles Izengo ameeleza kuwa tayari choo kimeshaanza kuchimbwa hivyo amewasihi wachimbaji kuendelea kutumia vyoo vya nyumba za wageni pindi wanaposubiri vyoo vya mgodi vikamilike.


Hata hivyo Afisa madini mkazi Mkoa wa kimadini Kahama Eng Joseph Kumburu amewataka uongozi wa mgodi kupanga maeneo ilikuweka mazingira salama pia washughulikie swala la vyoo haraka.


"Tumewambia mpange haya maeneo maduara yawe sehemu yake, muweke maeneo ya makazi na maeneo ya chakula maana ndio mazungira yenyewe pia kuwe na maeneo ya vyoo wasimamizi kuanzia kesho vyoo vianze kutengenezwa, hiyo ndio afya yenyewe", alisema Eng Kumburu.


Mgodi wa Nyikoboko mpaka sasa una wachimbaji wadogo zaidi ya elfu tatu.
Rehema Hasan mfanyabiashara wa chakula katika mgodi huo


Meneja wa Mgodi wa Nyikoboko Charles Izengo akielezea kuhusu usafi wa mazingira ya mgodi huo

katibu kamati ya ulinzi wa mgodi Sikujua Edward akizungumzia hali ya usalama


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso