Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga Josephat Mwaipaya akizungumza wakati wa kikao hicho.
Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga imekutana na wafanyabiashara na wajasiriamali waliopo mji mdogo wa Didia na Puni kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto wanazokumbana nazo sambamba na kutoa elimu.
Kikao hicho kimefanyika leo Julai 24, 2024 kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Kaimu Meneja wa Kodi kutoka TRA Shinyanga Ramadhan Omary ameeleza faida za matumizi ya mashine za risiti za kielektroniki (EFD) kwa wafanyabiashara na umuhimu wa kudai risisti kwa mteja aliyenunua bidhaa.
"Sisi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA jukumu letu ni kuhakikisha wafanyabiashara wanatoa risiti kwa wateja na wanunuzi wanadai risiti halali ya bidhaa waliyonunua ndio maana leo tumekuja kutoa elimu na kusikiliza changamoto za walipa kodi wetu ili kuboresha utoaji huduma kwenye mamlaka yetu", amesema Ramadhan Omary.
Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga Josephat Mwaipaya amesisitiza matumizi ya mashine za risiti za kielektroniki (EFD) wakati wa kufanya manunuzi kwa wafanyabiashara kwani ni takwa la kisheria.
"Sheria ya kodi inamtaka mnunuzi adai risiti halali kutoka kwa mfanyabiashara na asipofanya hivyo atakuwa amevunja sheria hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kutambua kuwa kudai na kutoa risiti halali ni wajubu wake, lengo likiwa ni kujenga nchi yetu kupitia mapato tunayokusanya", amesema Josephat Mwaipaya.
Nao baadhi ya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka mji mdogo wa Didia na Puni wameishukuru Mamlaka ya Mapato kwa kutoa elimu ya umuhimu wa matumizi ya mashine za risiti za kielektroniki (EFD) na kusikiliza changamato wanazokumbana nazo wakati wa ulipaji wa kodi.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga Josephat Mwaipaya akizungumza wakati wa kikao hicho.
Kaimu Meneja wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga Ramadhan Omary akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mmoja wa wafanyabiashara kutoka Mji Mdogo wa Didia akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mmoja wa wafanyabiashara kutoka Mji Mdogo wa Didia akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mmoja wa wafanyabiashara kutoka Mji Mdogo wa Didia akizungumza wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wafanyabiashara na wajasiriamali waliojitokeza kwenye kikao hicho.
Maafisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Shinyanga wakitoa huduma kwa wateja.
No comments:
Post a Comment