NA NEEMA NKUMBI HUHESO DIGITAL -KAHAMA
Club ya Young Africans Wilaya ya Kahama imefanya zoezi la usajili wa wanachama wapya wa Club hiyo Julai 18 katika uwanja wa Lumambo soko la Mkulima la zamani lililopo Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga
Zoezi hilo limeratibiwa na matawi mbalimbali ya Club ya Young Africans wilaya ya Kahama wakiwa na lengo la kuongeza wanachama wapya pamoja na kuwakumbusha wanachama kulipa ada na michango ya uanachama zoezi lililoongozwa na Kigerere gere ambaye alikuwa akihamasisha
wanachama kujisajili.
“Ukilipa ada ya uanachama utakuwa na uwezo wa kumbishia hata Magoma, sasa ukiwa hauna kadi utapata wapi ujasiri?, lakini ukiwa na kadi na unalipa ada unaweza ukamshusha na ukampandisha Magoma kwa sababu una ujasiri kwa kile unachokifanya” Amesema Kigere gere
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Matawi ya Young Africans sports club Wilaya ya Kahama ambaye pia ni mratibu wa Mashabiki na wanachama Mkoa wa Shinyanga Bwana Sebastian Mashinji maarufu kama komaa amesema kutokana na wanachama kutokulipa ada zao kwa mwaka uliopita Club hiyo ilipata hasara ya zaidi ya Bilion 1 ambapo amewataka wananchi kujisajiri na kulipia ada kwa wakati
“Juzi tulienda kwenye Mkutano Mkuu wa Club na baada ya taarifa tuliona kuwa Club imekosa makusanyo kutoka kwa wanachama na niwakumbushe wanachama kwamba siyo kujisajili tu wakumbuke na kulipa ada ya uanachama ambapo kujiunga ni Shilingi Elfu 29 na ada ni shilingi 24000 elfu Ishirini na nne kwa mwaka” Amesema Komaa
Hata hivyo Msemaji wa Vilabu vya Kahama Alfred Nyanda amesema wanaendelea kuhamasisha wanachama kujiunga na kuendelea kulipia ada zao ili kuwezesha kulipa wachezaji na kutambulika kikatiba.
“Tunaendelea kuhamasisha wananchi kulipa ada za uanachama pamoja na kujiunga kwani kama wananchi tukilipa ada kwa wakati tutaweza kumlipa Aziz Ki, Chama, Diarra, na wengine ambao wanaipa matokeo timu ya Young Africans” Amesema Nyanda
Kwa upande wa mwanachama wa Club ya Young Africans Josefu Lugeze kutoka Tawi la Kahama amesema mpira ni ajira hata ushabiki pia ni ajira maana inakusaidia kufahamiana na watu na kutengeneza fursa.
Pia mwanachama Shangwe Mfungo kutoka Tawi la Masumbwe Mbogwe Geita ameeleza faida wanazozipata ambazo ni kupata mikopo na fursa zaidi
Naye Himidi Rajabu kutoka Tawi la Kahama amesema wamefurahi kwa Club hiyo kujiandaa na kuleta usajili katika eneo lao kwani limeongeza hamasa kwa wanachama wapya na wale wanaolipa ada kutokana na faida wanazozipata ikiwa ni pamoja na punguzo la Asilimia 15% kwa matibabu ya mwanachama hai wa Club hiyo
Hata hivyo mdhamini wa Ligi Kuu nchini National Bank of Commerce (NBC) Ambayo ni Banki ya Taifa ya Biashara kupitia kwa Meneja Biashara wa Bank hiyo Wilaya ya Kahama Grace Siame amesema kupitia uanachama unaweza kupata kadi ya Benki ambayo imeunganishwa moja kwa moja na uanachama
“.... Unaweza kujipatia kadi ya Benki ya NBC ambayo inakuwa imeunganishwa moja kwa moja na uanachama wa Young Africans unapewa kadi ya ATM ambapo papo hapo inakuwa kama kadi ya Yanga” Amesema Siame
Wanachama wa yanya wakisubiri kusajiliwa
No comments:
Post a Comment