WAKALA wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA)Mkoa wa Shinyanga,wameanza maandalizi ya ujenzi wa daraja la mawe ambalo linaunganisha Kata ya Chibe na Oldshinyanga,pamoja na kunufaisha pia wakazi wote wa Mkoa wa Shinyanga.
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Meneja wa (TARURA)Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Avith Theodory,amesema daraja hilo litakuwa na urefu wa Mita 45 na gharama zake ni zaidi ya Milioni 120,ambalo litaimarisha mawasiliano na kuchochea uchumi kwa wananchi.
Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro alifanya ziara kukagua ujenzi wa daraja hilo na kutoa maagizo ujenzi wake uharakishwe ili wananchi wapate huduma.
No comments:
Post a Comment