SERIKALI imesema itaendelea kuboresha huduma za Mawasiliano hasa katika maeneo ya vijijini ili kufungua njia za Mawasiliono ya Simu pamoja na kuchochea shughuli za maendeleo kwa Wananchi.
Kauli hiyo imetolewa tarehe Julai 19, 2024, na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nauye (MB), alipotembelea kiijiji cha Ngokolo kilichopo Kata ya Bukomela Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga, wakati akikagua ujenzi wa Mnara wa Mawasiliano ya simu, ambapo amesema kuwa Serikali ipo kazini kuhakikisha Wananchi wanakuwa na mazingira bora ya mawasiliano.
Awali, Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani, amepongeza jitihada za Serikali kwa kuipatia Halmashauri hiyo kujengewa minara ya mawasiliano 7, ambapo minara 4 kati ya hiyo imekamilika huku akiomba Serikali kuongeza mingine ili kuwafikia Wananchi wa maeneo yote ya Ushetu.
Aidha, wananchi wa Kata ya Bukomela kwa nyakati tofauti wakizungumza, wameishukuru Serikali kupitia mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF)kwa kujengewa minara hiyo ambapo awali walikuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta wasiliano kwa kupanda milimani kwenye mawe na wengine juu ya miti.
Serikali imeendelea kushirikianna na Sekta binafsi za Mawasiliano kwa kutoa ruzuku katika ujenzi wa minara ya mawasiliano kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote
No comments:
Post a Comment