RWANDA KUPIGA KURA JULAI 15, KAGAME KUGOMBEA BILA KUPINGWA MIONGO MITATU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 15 July 2024

RWANDA KUPIGA KURA JULAI 15, KAGAME KUGOMBEA BILA KUPINGWA MIONGO MITATU




Raia wa Rwanda wanapiga kura Jumatatu ya Julai 15, 2024 katika uchaguzi ambao bila shaka utarefusha muda mrefu wa utawala wa Rais Paul Kagame, ambaye anagombea bila kupingwa baada ya miongo mitatu madarakani katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Wapinzani wake Frank Habineza wa Democratic Green Party of Rwanda na mgombea huru Philippe Mpayimana wamepata ushawishi mdogo sana kutoka kwa Raia na alikabiliana na wapinzani hao hao mwaka 2017, alipopata karibu asilimia 99 ya kura.

Wafuatiliaji wanasema matokeo kama hayo yanatarajiwa katika nchi ambayo upinzani mkubwa dhidi ya Kagame haujakuwepo kwa muda mrefu.

Kagame mwenye umri wa miaka 66, alichukua mamlaka kama kiongozi wa waasi waliochukua udhibiti wa serikali ya Rwanda na kumaliza mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Kagame alikuwa makamu wa rais wa Rwanda na kiongozi mkuu kutoka 1994 hadi 2000, alipokuwa rais kwa mara ya kwanza. Tangu wakati huo ametawala nchi hiyo ya Afrika Mashariki kama mtawala asiyevumilia upinzani wa kisiasa.

VOA Swahili

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso