MWANAFUNZI APATWA NA WASIWASI KUENDELEA NA MASOMO BAADA YA KUPORWA VIFAA VYA SHULE WAKATI AKIENDA SHULENI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 15 July 2024

MWANAFUNZI APATWA NA WASIWASI KUENDELEA NA MASOMO BAADA YA KUPORWA VIFAA VYA SHULE WAKATI AKIENDA SHULENI



Mwanafunzi Frank Emanuel Maduhu akitoka shule akiwa hana sare za shule na akiwa na madaftari mkononi

NA NEEMA NKUMBI HUHESO DIGITAL -KAHAMA

Mwanafunzi Frank Emanuel Maduhu wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Nyahanga, iliyopo Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, amelazimika kuhudhuria Shuleni bila sare za shule baada ya kuvamiwa na kundi la vibaka wiki hii na kuvuliwa nguo za shule viatu pamoja na begi la shule.


Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwao, mwanafunzi huyo amesema alifikwa na mkasa huo wiki hii, wakati akielekea shuleni, hali ambayo inampa wasiwasi kuendelea na masomo


Mama mzazi wa mtoto Frank, Angelina Mwandu amesema mwanae alirudi nyumbani bila nguo akiwa na majani kichwani huku akilia hali iliyompa wasiwasi ndipo alipoamua kwenda kutoa taarifa katika ofisi za serikali za mtaa pia shuleni.

"Mtoto wangu alirudi akiwa na majani kichwani huku akiwa hana viatu, nguo za shule na begi la shule nilipomuuliza amepatwa na nini akaniambia amekutana na kundi la vibaka ambao wamemfanyia hayo yote", alisema Angelina 

Yusuph Matondo mkazi wa kata ya Nyahanga  ameeleza kuwa kata ya nyahanga ni kubwa sana na shule ya sekondari iko kijiji kingine hivyo wanahitaji kuwa na sekondari ingine ili kuepusha matukio ya unyanyasaji kwa watoto kwani wanatembea umbali mrefu 
 
Mwananchi mwingine Happynes Mwabika amesema kijana anapambania elimu halafu anaporwa hilo ni takizo kubwa pia ameiomba serikali kuwawekea ulinzi watoto wao wanapoenda shule kwani shule iko mbali


Diwani Kata ya Nyahanga Pancraci Ikongoli amelaani tukio la mwanafunzi kuporwa vifaa vya shule pia amesema kuna sababu ya kuimarisha ulinzi hasa majira ya asubuhi wanafunzi wanapoenda shule. 

Sambamba na hilo diwani huyo amebainisha kwamba tayari wameshapata eneo kwa ajili ya kujenga shule hivyo wana wahamasisha wananchi kuanza kujenga shule nyingine ya sekondari ambayo itawasaidia wanafunzi kutopita katika mazingira hatarishi.

Diwani Kata ya Nyahanga  akilaani tukio lililompata mwana funzi Frank kwa kuporwa nguo za shule begi pamoja viatu na vibaka 


Mama mzazi wa mtoto Frank akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukuo lililompata mwanae

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso