Siku nne tangu kijana Shadrack Chaula [24] aliyechoma picha ya Rais kuhukumiwa kulipa faini ya Sh millioni 5 au kifungo cha miaka miwili jela , hatimaye michango ya wananchi imefanikiwa kumtoa katika Gereza la Ruanda Mkoa lililoko Mkoani Mbeya.
Shadrack aliyekamatwa kwa madai ya kuchoma picha ya Rais Samia Suluhu Hassan na kushitakiwa kwa kosa la kutoa taarifa za uongo, alikwenda Gerezaqni baada ya kushindwa kulipa faini hiyo.
Akizungumza baada ya kutoka katika Gerezani la Ruanda akiwa na ameambatana na Wakili wake Michael Mwangasa, Kijana huyo ambaye ni Msanii wa Sanaa ya uchoraji amewashukru Watanzania kwa kuchanga fedha na kumtoa Gerezani.
“Nawashukru Watanzania kwa upendo wa kunichangia Fedha na mawakili mlionihangaikia kuja kunitoa gerezani wote nawaombea kwa Mungu awabariki sana” amesema Shadrack huku akiwa na uso wa furaha.
Kwa upande wake, Wakili aliyekuwa
akishughulikia suala hilo, Michael Mwangasa amesema wana nia ya kukata Rufaa katika Mahakama kuu
kanda ya Mbeya
“Hatujaridhika na hukumu iliyotolewa kwa sasa tunaweka mambo sawa hasa taratibu zote za kisheria kabla ya kwenda kukata rufaa katika mahakama kuu kanda ya Mbeya” amesema Mwangasa
Kijana huyo alipofikishwa mahakamani, alisomewa shitaka la kutoa na
kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii TikTok, kosa ambalo ni
kinyume cha sheria ya makosa ya mtandao
kifungo cha 16
Hukumu
hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Mahakama ya wilaya Rungwe Mkoa wa Mbeya, Shamla
Shehagilo, baada ya mshitakiwa huyo, mkazi wa kijij cha Ntokela, Wilayani humo kukiri kosa hilo.
Baada
ya kukiri ya kosa hilo, Hakimu Shehagilo alimtia hatiani kwa kosa hilo na
kumuhukumu kulipa faini Sh millioni 5 au
kwenda jela miaka miwili.
Awali, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Rosemary Mgenije, aliyekuwa akisaidiana na wakili Veronica Mtafya, alidai juni, 22, 2024 eneo Ntokela lililopo kata ya ndato wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya, mshitakiwa alitenda kosa hilo kupitia akaunti yake ya mtandao kijamii@jet.fightershop akiwa ameshika picha inayomwonesha Rais Samia, Akisema
“Kwa kuwa umeshindwa kutetea haki Taifa lako lisiathirike na ushoga, hii video inakuhusu wewe na si mtu mwingine wakati ukijua taarifa hizo ni uongo na upotoshaji kwa jamii” amedai Wakili Veronica
No comments:
Post a Comment