MHE.MAKAMBA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 26 WA KAMATI YA MAWAZIRI WA ASASI YA SIASA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 12 July 2024

MHE.MAKAMBA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 26 WA KAMATI YA MAWAZIRI WA ASASI YA SIASA




Mhe. January Makamba (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 26 wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC. Mkutano huo unaofanyika Lusaka, Zambia Julai 11 - 12, 2024 ulifunguliwa rasmi na Mhe. Mulambo Haimbe, SC, (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Zambia ambaye kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Mawaziri (MCO).


Mkutano huu umehudhuriwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kutoka nchi wanachama wa SADC ambao wana jukumu la kusimamia Amani na Usalama.


Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Rashid Hamduni ni miongoni mwa ujumbe wa Tanzania katika mkutano huu ambao ajenda kuhusu mapambano dhidi ya rushwa kupitia utekelezaji wa Mpango Mkakati na Mpango Kazi wa SADC Dhidi ya Rushwa wa mwaka 2023 - 2027 ilijadiliwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso