MADIWANI SHINYANGA WATAKA WAKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI WA BARABARA KWA WAKATI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 30 July 2024

MADIWANI SHINYANGA WATAKA WAKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI WA BARABARA KWA WAKATI



Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog


Baraza la Madiwani Manisipaa ya Shinyanga limewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya Barabara katika Manispaa ya Shinyanga kupitia Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kukamilisha ujenzi wa barabara hizo kwa wakati kulingana na mikataba yao.


Madiwani wamebainisha hayo leo Julai 30,2024 katika kikao cha baraza la madiwani kilichoketi kupokea taarifa kutoka Taasisi za Serikali pamoja na kamati za kudumu za baraza hilo.


Kupitia kikao hicho madiwani wamesema wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara wamekuwa wakikiuka mikataba hivyo kuchelewa kukamilisha kumaliza barabara hizo.


"Kuna kivuko ambacho kinatoka Mwamala Masekelo kuelekea katika kata ya Ibinzamata, Kitangili pamoja na Kizumbi kivuko hiki ni chamuhimu sana kwasababu kinaunganganiisha kata hizo, Mwaka 2015 kuna wanafunzi wawili walifariki dunia kutokana na kivuko hicho, tulipata barua tarehe 26/06 /2024 ya kuanza kutengeneza kivuko hicho lakini mpaka sasa hakuna chochote kinaendelea", amesema Peter Koliba Diwani wa kata ya Masekelo.


"Kuna Mkandarasi anaitwa UK anayetekeleza mradi kata ya Kizumbi Mkataba umeisha tangu tarehe 29/07/2024 mpaka sasa kazi haijaisha sasa kuna njia gani nyingine ya kutusaidia ili wananchi hao wapate huduma ya barabara kwa haraka? ", amehoji Mhe, Reuben Kitinya Diwani wa kata ya Kizumbi.




Akitoa ufafanuzi wa kuchelewa kwa kukamilika kwa barabara hizo Kaimu Meneja TARURA wilaya ya Shinyanga Mhandisi Yohana William amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 walitengewa Shilingi bilioni 2,932,810,000.00/= kwa ajili ya ujenzi miundombinu ya barabara lakini pesa zilizofika na kufanya kazi ni milioni 918,917,000.00 sawa na asilimia 31.33 ya fedha hizo.


Aidha amesema maeneo ya barabara ambayo hayakufanyiwa ukarabati au maboresho kwa mwaka wa fedha 2023/2024 yatapewa kipaumbele katika utekelezaji wa mwaka wa fedha 2024/2025.


Akizungumzia changamoto hiyo msitahiki Meya Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko amesema kutokamilika kwa baadhi ya barabara zilizpanza kufanyiwa marekebisho ni kutokana na wakandarasi hao kutolipwa stahiki zao.




"Kama fedha zingekuwepo hoja zote hizi zisingekuwepo kwa mwaka wa fedha 2023/2024 wakandarasi wanadai stahiki zao, hivyo tunatakiwa tuwapongeze TARURA kufanya kazi katika mazingira ya namna hiyo",amesema Mstahiki Meya Manispaa ya Shinyanga Mhe, Masumbuko.






No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso