Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi kutambua kwamba madaraka ni sawa na nguo ya kuazima ambayo wakati wowote Mmiliki wa nguo anaweza kuichukua hivyo amewasihi Viongozi kutanguliza maslahi ya Taifa kwanza kabla ya kutanguliza maslahi yao.
Akiongea Ikulu Dar es salaam leo July 26,2024 baada ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali, Rais Samia amesema “Sitarajii muende mukazidhihaki Wananchi au kuwadogosha Wananchi kwasababu wao ndio sababu ya sisi kuwepo hapa, nendeni mkawatumikie, tumieni Mamlaka zenu kwenda kuwatumikia Wananchi, hakikisheni maslahi ya Wananchi yanapatikana, kiapo kinapiga ukikiendea upande hakitokuacha kitakupiga, ukikidhihaki kitakupiga, kwahiyo nendeni mkaishi na viapo vyenu”
“Kila tunayemtumikia, kila anayeitwa Mtanzania, heshima na utu wake ni sisi wa kuutumikia kwahiyo nendeni mkatumikie Wananchi, kiapo kinasema hutoendekeza mambo yako binafsi kabla ya yale ya Taifa kwahiyo hilo nendeni mkalitazame, ukifika hapo maslahi yako binafsi kama Binadamu sawa lakini mbele maslahi ya Taifa, sasa wale mliozoea kutumia nafasi zenu kujinyanyua nyinyi kabla ya kunyanyua Taifa naomba kama upo kwenye madaraka rekebisha kabla sijakuona lakini kama ndio unaingia tambua hilo kwamba maslahi yako baadaye maslahi ya Taifa mbele”
“Nihitimishe kwa kuwaambia madaraka haya ni dhamana na dhamana inataka kufanyiwa kazi na kila mmoja awajibike kwa mwenendo, matendo na kauli njema, sasa Waswahili pia wanasema madaraka haya ni nguo ya kuazima ukiitumia vizuri mwenyewe anakuona unavaa vizuri haufanyi utovu wa adabu huko nje unakwenda unarudi vizuri anaweza akakustahimilia hata wili Wiki wiki tatu ukabakia na nguo yake anakutazama lakini akibaini na unatovuka adabu kwa nguo yake aliyokuazima atachukua nguo yake, madaraka haya ni nguo ya kuazima haisitiri mambo, saa yoyote inaweza ikakuvuka kwahiyo niwaombe twendeni tukaweke heshima kama kanuni, miongozo na sheria zetu zinavyotutaka”
No comments:
Post a Comment