HALMASHAURI AMBAZO HAZIJAANZISHA VITUO VYA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI ZIANZISHE VITUO HIVYO- PROF. AURELIA KAMUZORA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 3 July 2024

HALMASHAURI AMBAZO HAZIJAANZISHA VITUO VYA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI ZIANZISHE VITUO HIVYO- PROF. AURELIA KAMUZORA

Mwenyekiti wa Baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) Prof.Aurelia Kamuzora akizungumza na watoa huduma katika kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi kilichopo katika Manispaa ya Kahama mkoa wa Shinyanga

NA NEEMA NKUMBI HUHESO DIGITAL- KAHAMA

Mwenyekiti wa Baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) Prof.Aurelia Kamuzora ametoa wito kwa Halmashauri ambazo hazijaanzisha vituo vya uwezeshaji wananchi kichumi kuanzisha vituo hivyo ili kutoa fursa na elimu mbalimbali ikiwemo elimu ya mifumo ya matumizi ya Tehama kwa faida ya halmashauri zao na jamii kwa ujumla katika kukuza uchumi.


Wito huo umetolewa julai 3 wakati akizungumza na watoa huduma katika kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi kilichopo katika Manispaa ya Kahama mkoa wa Shinyanga


Prof.Kamuzora amesema kuwa uwepo wa vituo vya uwezeshaji wananchi kiuchumi una faida kubwa katika kumuwezesha mtanzania kuwa na uchumi unaolingana na maendeleo ya sasa na kutoa wito kwa viongozi kutembelea kituo cha Kahama kujifunza kwa vitendo.

"Hiki kituo ni cha muhimu sana sababu kinatoa hizo huduma wataweza kufanya biashara kwa maana biashara sasa hivi ni ya kimtandao kwa hiyo nawaomba viongozi wote wa halmashauri waanzishe vituo kama hivi na tunawakaribisha sana Kahama waje waone mfano halisi jinsi tunavyoweza kukuza uchumi pamoja na kuwawezesha wananchi kuwa ni sehemu ya uchumi" alisema Prof Kamuzora


Naye Msimamizi wa kituo cha uwezeshaji wananchi Kiuchumi tawi la Kahama Jozaka Bukuku amesema kuwa kituo hicho kinawatoa huduma wanaotoa mikopo kwa makundi mbalimbali ikiwemo mikopo ya Fedha ambapo kati ya mwezi April hadi june 2024 jumla ya Shilingi milioni 517.6 zimetolewa na kutoa ombi kwa baraza la uwezeshaji kuziingiza baadhi ya taasisi muhimu katika kituo hicho wakiwemo OSHA.


Aidha Katibu mtendaji wa baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi. Beng’i Issa ametoa wito kwa wananchi wa Manispaa ya Kahama kujitokeza kwa wingi katika kituo hicho ili kusaidiwa kuboresha Uchumi wako huku baadhi ya wananchi wanaopata huduma katika kituo hicho wakielezea manufaa ya uwepo wa kituo cha uwezeshaaji wananchi kiuchumi.

Msimamizi wa kituo cha uwezeshaji wananchi Kiuchumi tawi la Kahama Jozaka Bukuku




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso