DKT.MWINYI AKUTANA NA WABUNGE WA MAREKANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 16 July 2024

DKT.MWINYI AKUTANA NA WABUNGE WA MAREKANI

 





Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema uchumi wa Zanzibar unategemea utalii, na kuwa watalii kutoka Marekani wameongezeka nchini.


Rais Dkt.Mwinyi aliyasema hayo alipokutana na Ujumbe wa Wabunge wa Marekani ukiongozwa na Mhe.Katherine Clark waliofika Ikulu Zanzibar tarehe 16 Julai 2024.


Aidha Rais Dk.Mwinyi ameshukuru ushirikiano uliopo na Marekani katika miradi mbalimbali ya maendeleo pia alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka Marekani kuwekeza kwenye sekta ya uchumi wa buluu.


Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema Zanzibar ina amani na utulivu kutokana na kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.


Naye Katherine Clark ameeleza kuwa Marekani itaisaidia Zanzibar katika uwezeshaji wa Wanawake hususani wakulima wa Mwani na vyuo vya ufundi na mafunzo ya amali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso