DKT.MWINYI AKUTANA NA UONGOZI WA ZRCP - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 17 July 2024

DKT.MWINYI AKUTANA NA UONGOZI WA ZRCP




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema lazima yafanyike mabadiliko katika uendeshaji wa Serikali ili kuendana na mageuzi ya uchumi wa kidijitali




Rais Dkt.Mwinyi aliyasema hayo leo tarehe 17 Julai 2024, alipokutana na Uongozi wa Kituo cha utafiti wa sera na uchambuzi Zanzibar (ZRCP) ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Juma Hassan Reli Ikulu Zanzibar.


Aidha Rais Dkt.Mwinyi amewataka ZRCP kutafuta njia mbadala wa kusimamia utekelezaji wa tafiti zinazofanyika katika sekta mbalimbali.


Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amekubali ombi la ZRCP kushiriki kufungua Mkutano wao mkuu wa mwaka utaofanyika tarehe 5 Septemba 2024.


Naye Juma Hassan Reli ameeleza kuwa miradi ya maendeleo imetekelezwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya nane chini ya Rais Dkt.Mwinyi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso