DKT.MWINYI AFUNGUA MKUTANO WA WAZALISHAJI SUKARI SADC - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 10 July 2024

DKT.MWINYI AFUNGUA MKUTANO WA WAZALISHAJI SUKARI SADC


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Tanzania sekta ya sukari ni kipaumbele katika kilimo kwa kuwa viwanda vya sukari ni vitovu vya kilimo na uchumi.

Rais Dkt.Mwinyi aliyasema hayo alipofungua mkutano wa wazalishaji sukari wa nchi za SADC katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Zanzibar Airport, tarehe 10 Julai 2024.


Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Tanzania imeweka mazingira wezeshi ya uwekezaji katika kilimo cha Miwa na uzalishaji sukari.


Rais Dkt.Mwinyi ametoa rai kwa nchi za SADC kutumia fursa zilizopo kwa kuweka mazingira bora zaidi ya uwekezaji ili kukuza uzalishaji wa Sukari.


Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa washiriki wa mkutano huo wa siku moja kuwekeza kikamilifu katika teknolojia za kisasa na mbinu za kilimo za kisasa zinazoongeza tija ili kuboresha mavuno ya miwa na uzalishaji sukari Afrika.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso