BIMA YA AFYA SULUHISHO LA HUDUMA BORA ZA AFYA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 14 July 2024

BIMA YA AFYA SULUHISHO LA HUDUMA BORA ZA AFYA

 





Na Majid Abdulkarim, KATAVI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kujiunga na huduma ya Bima ya afya kwa wote ili kuzidi kuimarisha huduma za Afya nchini


Pia Mhe. Rais amewataka wananchi wa Katavi kuuza mazao ili waweze kupata fedha na kujiunga na mfuko wa bima ya afya kwa wote.


Kauli hiyo ameitoa Julai 13, 2024 wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Serikali wakati wa kilele cha wiki ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi kilichohitimishwa mkoani Katavi


Dkt Samia amesema Serikali imeendelea kuweka misingi madhubiti ya vyanzo vya uhakika vya fedha ili kutekeleza bima ya afya kwa wote.


Amesema gharama za matibabu kwa sasa zimekuwa juu na suluhisho ni bima ya afya kwa wote.


"Niwaombe sana ndugu zangu wa Katavi unajua wakati mwingine umaskini ukiukumbatia na wenyewe unakukumbatia mnapouza mazao jitahidini kuhakikisha mnajiunga na bima ya afya kwa wote uweze unatibiwa mwaka mzima bila usumbufu" amesema Mhe. Rais na kuongeza


"Tukifanya hivyo watanzania wote tutapata fursa ya kupata matibabu mazuri na ya viwango kulingana na uwekezaji mkubwa ulofanywanaSerikali yenu,"amesisitiza Dkt Samia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso