ATUPWA JELA MIAKA MIWILI KWA KOSA LA KUCHOMA MOTO PICHA YA RAIS SAMIA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 5 July 2024

ATUPWA JELA MIAKA MIWILI KWA KOSA LA KUCHOMA MOTO PICHA YA RAIS SAMIA


Mahakama ya Hakimu mkazi wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya imemhukumu Msanii wa Sanaa ya uchoraji Shedrack Chaula [24] kutumikia kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh. Million 5 baada ya kukutwa na hatia ya kusambaza taarifa za uongo dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan.


Upande wa Jamhuli ukiongozwa na Wakili wa Serikali Rosemary Mginye na Veronica Mtafya umeieleza Mahakama hiyo kuwa mshitakiwa ametenda kosa la kusambaza taarifa za uongo kupitia Mtandao wa Tiktok na huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha Sheria Kifungo cha 16 cha Sheria ya makosa ya Mtandaoni.


Baada ya Hukumu hiyo iliyotolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Ramla Shagilo mshitakiwa alipewa nafasi ya kujitetea hata hivyo aligoma kufanya hivyo licha ya kukiri kutenda kosa hilo.


Baada ya Mshitakiwa kukosa pesa za faini amepelekwa katika Gereza la tukuyu na kuanza kutumikia adhabu yake.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso