WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI IMEKABIDHIWA KOMBE NA CHETI BAADA YA KUIBUKA WASHINDI UTOAJI TAARIFA KWA UMMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 22 June 2024

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI IMEKABIDHIWA KOMBE NA CHETI BAADA YA KUIBUKA WASHINDI UTOAJI TAARIFA KWA UMMA







Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi leo imekabidhiwa Kikombe na Cheti baada ya Kuibuka mshindi wa pili katika utoaji wa taarifa kwa Umma katika kipindi cha mwaka 2023/2024.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeibuka na ushindi huo wa pili kati ya Wizara Kumi Bora na kati ya Wizara 26 za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tuzo hizo zimekabidhiwa leo na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye wakati akifunga Kikao Kazi cha 19 cha Maafisa Habari wa Serikali, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso