Sheikh Ally Muhidiin Mkoyogole Mjumbe wa baraza la Ulamaa Bakwata Taifa katika baraza la idd lililofanyika katika Msikiti wa Mwendakulima kata ya Mwendakulima Manispaa ya Kahama akizungumza waumini wa dini ya Kiislamu nchini.
NA NEEMA NKUMBI HUHESO DIGITAL- KAHAMA
Waumini wa Dini ya Kiislamu nchini wameaswa kuwathamini waalimu wa madrasa kwa kuhakikisha Sheikh au Ostaz anafaidika kupitia nafasi zao pia kuwafuatilia waalimu pamoja na wanafunzi maendeleo yao ya madrasa.
Wito huo umetolewa juni 20, 2024 na Sheikh Ally Muhidiin Mkoyogole Mjumbe wa baraza la Ulamaa Bakwata Taifa katika baraza la idd lililofanyika katika Msikiti wa Mwendakulima kata ya Mwendakulima Manispaa ya Kahama.
"Elimu ni dini tutazame wapi tunaenda kuchukua elimu yetu wazazi kazi yao kuwangalia Sheikh au ostaz kwa ile kazi yao wanayoifanya na kuangalia madrasa inafanyaje, nakufatilia tabia za waalimu na wanafunzi", alisema Sheikh Ally Muhidiin
Hassan Mrisho ni muumuni wa Dini ya Kiislamu Mwendakulima amesema wajibu wao kama wazazi ni kumlinda mwalimu kwa hali na mali kwa kuchanga chochote walichonacho kwa sababu wanaisaidia nchi kuwa katika hali ya salama.
Muumini mwingine Fatuma Salimu amesema walimu wana umuhimu kwa sababu wanafundisha maadili mema pia amewashauri waumini wenzake kujitoa kwa moyo Mwalimu ili na yeye awasaidie wao.
Naye mwalimu wa madrasa Abbas Abdallah ameeleza umuhimu wa waalimu katika Serikali na duniani kote ni kumjenga mwananchi au mtoto katika maadili mema na kuijenga nchi pia .
"Umuhimu wa waalimu duniani kote ni kumjenga mwananchi au mtoto katika maadili mema pili atasaidia kumjenga nchi yake, tunashuhudia viongozi wanapata tabu kwa kukosa uadilifu", alisema Abbas Abdallah
Awali akimkaribisha mgeni rasmi sheikh wa wilaya ya Kahama Alhaji Omary Adam Damka, aliwataka wazazi/walezi wilayani humo kuthamini elimu ya dini na ya dunia hususan kwa watoto wa kike, ambao wamekuwa wahanga wa ndoa za utotoni kwa tamaa za mali kwa wazazi/walezi wao.
"Tusibague watoto wa kuwapeleka shuleni, watoto wa kike wasomeshwe na wa kiume wasomeshwe, tumekuwa tuna kasumba moja katika maeneo yetu ya bara kukimbilia kuwaozesha watoto wetu wa kike pasi na kuhakikisha kwamba elimu zao wamefikia kiwango gani, Mtume Muhammad (S.A.W) anasema kutafuta elimu ni lazima kwa kila muislamu mwanaume na mwanamke" Alisema Sheikh Damka.
Sheikh wa wilaya ya Kahama Alhaji Omary Adam Damka, Akizungumza waumini wa dini ya kiislamu wilayani humo akiwataka kuthamini elimu ya dini na ya dunia
Imamu wa msikiti wa mwendakulima Manispaa ya Kahama Sheikh Issa Kamwendo akizungumza wakati wa baraza la idd
TAZAMA PICHA ZAIDI
Picha na Neema Nkumbi
No comments:
Post a Comment