Afisa madini mkazi wa mkoa wa kimadini Kahama Eng Joseph Kumburu wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wadogo kwenye semina ya elimu ya mialo iliyofanyika katika Kijiji cha Wisolele, mgodi wa Ntambalale kata ya Segese Halmashauri ya Msalala
NA NEEMA NKUMBI HUHESO DIGITAL- KAHAMA
Wachimbaji wadogo wadogo wa madini ya dhahabu katika mkoa wa kimadini Kahama wametakiwa kufuata utaratibu wa uuzaji wa madini, ikiwa ni Pamoja na utunzaji wa kumbukumbu ili kuepuka kukwepa kulipa kodi ya serikali.
Wito huo umetolewa na Afisa madini mkazi wa mkoa wa kimadini Kahama Eng Joseph Kumburu wakati akizungumza kwenye semina ya elimu ya mialo iliyofanyika katika Kijiji cha Wisolele, mgodi wa Ntambalale kata ya Segese Halmashauri ya Msalala, kutokana na kuwepo kwa wanunuzi wa dhahabu wasio rasmi katika maeneo ya wachimbaji hao, hali inayosababisha upotevu wa kodi za serikali.
Nae afisa wa TAKUKURU kutoka wilaya ya Kahama Mlamzi Pius Kuhanda amewaasa wachimbaji hao kuepuka rushwa maeneo ya migodini kwani inaikosesha serikali mapato.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Jaffary Katimba amesema kulipa kodi ni sehemu ya maendeleo ya nchi kila anaefanya biashara awajibike kulipa kodi ili kujenga nchi kwa kukusanya mapato, pia amewataka wafanya biashara kuwa na vibali halali.
Ezekiel Kasala mchimbaji mdogo katika mgodi wa Tambalale ameiomba ofisi ya madini kupeleka jiko la kuchoma dhahabu kwenye eneo la mgodi kwa ajili ya kuchoma dhahabu ili kuepusha gharama za nauli pale wanapokuwa wanafuata huduma mjini
Wachimbaji wadogo wadogo wa madini ya dhahabu katika mkoa wa kimadini Kahama wakipewa elimu juu ya ulipaji wa kodi
No comments:
Post a Comment