Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 02, 2024 amezindua jengo la kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi katika halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale, Mkoani Geita.
Jengo hilo ambalo limejengwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lililopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wakazi wa eneo hilo kutumia fursa hiyo kupata elimu ya biashara na ujasiriamali pamoja na mikopo ili wajiendeleze kiuchumi.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wananchi hao kuunda vikundi ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na Serikali. “Vikundi vinakopesheka kwa urahisi hata anuani yake ni rahisi pia”.
Kwa Upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Ummy Nderiananga amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga fedha kwenye Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ambayo imewawezesha kutekeleza programu mbalimbali za uwezeshaji wananchi kiuchumi
“Mheshimiwa Waziri Mkuu tutaendelea kulisimamia Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ili liweze kufanya vizuri katika uwezeshaji wananchi kiuchumi”
No comments:
Post a Comment