TFF IMEKABIDHI VIFAA MIPIRA 50 UMITASHUMITA NA UMISSETA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 10 June 2024

TFF IMEKABIDHI VIFAA MIPIRA 50 UMITASHUMITA NA UMISSETA




Shirikisho la soka nchini (TFF) limekabidhi mipira 50 itakayotumika kwenye Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) yanayoendelea mkoani Tabora.


Makabidhiano ya mipira hiyo yamefanyika leo Juni 10, 2024 kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Tabora wavulana, yakiongozwa na kocha wa Soka kutoka TFF, Boniface Pawasa aliyemwakilisha Mkurugenzi wa ufundi kutoka shirikisho hilo Oscar Mirambo.

Akizungumza baada ya kupokea mipira hiyo, Mratibu wa michezo ofisi ya Rais TAMISEMI, Yusuph Singo amesema vifaa hivyo vitaongeza ufanisi wa mashindano hayo na kuzidi kuyapa thamani.

“Kama ambavyo nimekuwa nikisema kuwa mashindano ya mwaka huu ni ya kipekee kutokana na maandalizi yake lakini pia maboresho makubwa ambayo yamekuwa yakiendelea ikiwepo kuwasili kwa vifaa vya michezo kama hivi”, amesema Singo.

Kwa upande wake Boniface Pawasa ameeleza kuwa TFF itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI, kutokana na mikakati mizuri ambayo imeelekezwa kwenye kukuza soka la vijana hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso