Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dkt. Mzee Suleiman Mndewa amehimiza matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma za Posta ili kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia duniani.
Amesema matumizi ya teknolojia yanarahisisha maisha na kupunguza gharama za usafirishaji pamoja na kuleta ufanisi wa huduma za usafirishaji kwa njia ya Posta kwa sababu Dunia ipo kwenye uchumi wa kidigiti.
Dkt. Mzee ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) unaofanyika kuanzia tarehe 3- 14 Juni, 2024, jijini Arusha yalipo Makao Makuu ya Ofisi za PAPU, na kuwakutanisha wataalamu kutoka nchi wanachama wa PAPU pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya posta kutoka barani Afrika na Umoja wa Posta Duniani.
No comments:
Post a Comment