NA NEEMA NKUMBI HUHESO DIGITAL-KAHAMA
Picha ya miti iliyokatwa kwa ajili ya kutengeneza madawati
Upandaji miti ni shughuli yenye faida nyingi kwa jamii, hasa katika shule za msingi kama Mhongolo, ambapo umeleta mabadiliko chanya kwa wanafunzi.
Hivi karibuni, shule ya Msingi Mhongolo imeweza kupata madawati hamsini na meza mbili za walimu baada ya kukata miti 29 iliyokuwa imepandwa hapo, Huu ni mfano mzuri wa jinsi rasilimali za asili zinavyoweza kutumika kuboresha mazingira ya kujifunzia.
Mwenyekiti wa mtaa wa Mhongolo, Emanuel Nangali, amesema kuwa madawati haya yamepatikana baada ya juhudi za pamoja kati ya kamati ya shule, serikali ya mtaa, na walimu kukubaliana kukata miti iliyopandwa shuleni hapo ili wapate madawati.
Nangale ameongeza kuwa Mti uliokuwa unachukua nafasi isiyohitajika umesaidia kutatua uhaba wa madawati, ambapo wanafunzi wengi walikosa mahali pa kukalia darasani sasa wanakaa katika madawati hayo yaliyotokana na miti ya shule, hali hii inaonyesha umuhimu wa ushirikiano katika masuala ya maendeleo.
Clement Masonga, Mwenyekiti Msaidizi wa kamati ya shule, ameelezea kuwa waliomba kibali cha kukata miti ili kutengeneza madawati, baada ya kupata kibali, walifanya makubaliano na mhandisi wa madawati ambao walikubali kutumia miti hiyo, Hii inaonyesha jinsi jamii inavyoweza kushirikiana katika kutatua matatizo yao wenyewe.
Mkuu wa shule, Enest Peter, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano huo na kupongeza hatua iliyofikiwa kwamba wanafunzi hawatakaa tena chini.
Mwalimu Ernest ameongeza kuwa wanafunzi wapatao elfu mbili mia tano, bado wanakabiliwa na uhaba wa walimu na matundu ya choo umeendelea kuwa changamoto.
Pia ameiomba serikali kuongeza idadi ya walimu kutoka thelathini na tano waliopo ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.
Neema Jacob, mwanafunzi wa darasa la sita amepongeza juhudi hizo za upatikanaji wa madawati pia amewasihi wanafunzi wenzake kutunza miti kwani miti ina matunda mengi ambapo imewasaidia wao kupata madawati kupitia miti iliyopandwa shuleni hapo.
Shule ya Msingi Mhongolo imeonyesha mfano jinsi upandaji miti unavyoweza kuwa na faida si tu kwa mazingira, bali pia kwa elimu na ustawi wa jamii pia Ushirikiano wa jamii, serikali, na shule unahitajika ili kutatua changamoto na kuendelea kuleta maendeleo katika sekta ya elimu.
Mwenyekiti wa mtaa wa Mhongolo akizungumza na Huheso Digital
Baadhi ya miti inayopatikana katika shule ya Mhongolo
Mkuu wa shule aliyevaa miwani na pembeni ni mwenyekiti wa mtaa wakikabidhiwa madawati na aliyeyatengeneza
No comments:
Post a Comment