Wizara ya Ardhi, Nyumba Maendeleo ya Makazi Mkoa wa Mwanza kupitia office ya Kamishina Msaidizi ambae ni Happiness Mtutwa Imewataka Wananchi wa Mkoa wa Mwanza kulipa Kodi ya Ardhi kwa wakati
Akizungumza Happiness na Waandisi wa Habari amesema Wananchi wengi wanachanganya Kodi ya Ardhi na Kodi ya Majengo, hivyo bhac Wananchi wanatakiwa kujua Kodi ya Ardhi Inalipwa Office za Ardhi za Mkoa, Halmashauri na Wilayani , Kodi za Majengo zinalipwa TRA kupitia Njia ya Luku.
Hivyo ni wajibu wa Kila Mwananchi kulipa Kodi ya Kampuni, Viwanja, Taasisi za Umma na Binafsi kutolipa Kodi za Ardhi kunaweza kupelekea kunyanganywa Eneo lako,lakini pia kufikishwa Mahakamani ambapo unaweza kufutiwa Umiliki wa hati yako.
Niwaombe Wananchi wa Mkoa wa Mwanza walipe Kodi ya Ardhi Kwa wakati Ili kuondoa Usumbufu unaoweza kujitokeza.
Serikali ya awamu ya Sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassani Amewapendelea wananchi wa Mkoa Mwanza, Tumepata ugeni wa Viongozi kutoka Sehemu Mbalimbali Wakiongozwa na Mhe, Waziri wa Ardhi Jerry Silaa lakini Pia na Naibu Waziri wake Pamoja na Viongozi wengine kutoka makao makuu mpaka Sasa wanaendelea na Zoezi la upimaji wa Viwanja Mkoani Mwanza.
No comments:
Post a Comment