Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) Shaaban Matwebe
Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) kwa kushirikiana na Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (TAHLISO) imeandaa Kongamano la Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii nchini litakalofanyika tarehe 20/5/2024 kwenye ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti JUMIKITA, Shaaban Matwebe amesema Kongamano hilo linalotarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 500, litaongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.
"JUMIKITA inapenda kuutaarifu umma kuwa, Kongamano hilo litakuwa na dhima kuu ya kujadili uandishi wa habari kupitia mitandao ya kijamiii pamoja na upashanaji wa habari kupitia mitandao hiyo. Pamoja na dhima hiyo kuu, Kongamano hilo litajadili mafanikio ya miaka mitatu ya serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni pamoja na maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani. JUMIKITA inawakaribisha wote kwenye Kongamano hili muhimu kwa ustawi wa nchi yetu",amesema Matwebe.
Amesema mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii na uzalendo, fursa zilizopo kwenye tasnia hii, mafanikio na changamoto ili kutoa mchango wa kiundeshaji kwa wadau kupitia JUMIKITA na mapendekezo yatakayosaidia serikali kwenye uratibu wa sera za jinsi ya kuunganisha sayansi ya uchumi wa taarifa (information economics) na uchumi wa taarifa (information economy).
No comments:
Post a Comment