Tanzania imeungana na nchi nyingine duniani katika Kongamano la 10 la Maji Duniani (10th World Water Forum) ambalo limepitisha Azimio la Mawaziri (Ministerial Declaration on Water for Shared Prosperity).
Azimio hilo ambalo
msingi wake ni mikataba na maazimio mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kuhusu maji
kama vile Maji ni Haki ya Binadamu limeibua changamoto za maji duniani kama
vile mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kasi ndogo ya dunia kulifikia lengo
namba 6 la Malengo ya Endelevu ya Umoja wa Mataifa linalohusu maji.
Aidha, Azimio hilo linatoa hamasa ya kutatua changamoto hizo kwa kuwa na ubunifu na uendelevu wa upatikanaji wa fedha za maji (innovative and sustainable financing) pamoja na uongozi na utashi wa kisiasa
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan katika kongamano hilo la Maji la kumi duniani lililohusisha wakuu wa nchi mbalimbali pamoja na mawaziri na wawakilishi wa mataifa mbalimbali.
No comments:
Post a Comment