WATU 11 WAFARIKI DUNIA BAADA YA MTAMBO WA KIWANDA CHA MTIBWA SUGAR KULIPUKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 23 May 2024

WATU 11 WAFARIKI DUNIA BAADA YA MTAMBO WA KIWANDA CHA MTIBWA SUGAR KULIPUKA

Watu 11 wamefariki Dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada hitilafu iliyotokea katika mtambo wa mvuke wa kuzalisha umeme katika kiwanda Cha kuzalisha Sukari Mtibwa Suger kilichopo Tuliani Wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro


Kwa mjibu wa Kamanda wa zimamoto na uokoaji Mkoa wa Morogoro, Shabani Marugojo amesema tukio hilo limetokea Saa 7:30 Usiku kuamkia leo Mei 23, 2024, huku chanzo bado hakijafahamika


“kulitokea hitilafu katika mtambo wa mvuke wa kuzalisha umeme Waliofariki ni Wataalamu wa Umeme na Mitambo ambao walikuwa kwenye chumba cha kudhibiti mitambo hiyo” amesema Kamanda huyo

 

 

Amesema kati ya waliofariki kuna Raia watatu wa kigeni kutoka Kenya, India na Brazil ambapo miili ya wote waliopoteza Maisha imehifadhiwa Hospitali ya Mtibwa Sugar huku majeruhi wawili wakiwa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni ya Bwagala

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso