Wanafunzi wa vyuo vikuu wamepongeza jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa jitihada zake katika kuboresha miundombinu ya elimu ya juu wakidai kuwa imewatengenezea mazingira mazuri ya kujisomea.
Hatua hii inakuja baada Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2024/25, ambapo imepanga kutekeleza vipaumbele vitano vyenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kuwezesha vijana wa kitanzania kupata maarifa, ujuzi, kujiamini, kujiajiri na kuajirika.
Mmoja kati ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Ardhi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Jinsia na Makundi Maaalum katika Serikali ya chuo hicho, Caro Francis amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuwatengenezea mazingira rafiki wanafunzi wa elimu ya juu.
"Utekelezaji wa miundombinu ya ujenzi chuo kikuu cha Ardhi umefanyika kwa 48%, kwa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya Ujenzi umekamilika kwa 43%, unaweza ukaona ni kwa namna gani wanafunzi tunanufaika"
No comments:
Post a Comment