MENEJA wa Yanga, Walter Harson, amesema majukumu aliyonayo kwa sasa Yanga hawezi kushughulika na masuala ya uwakala wa wachezaji, hajawahi na hakuna mchezaji anayemsimamia.
Akizungumza na HabariLEO, Walter amesema suala la uwakala wa wachezaji limekaa kimgongano wa maslahi, hivyo sio kiongozi ambaye anaweza kuhusika na masuala ya uwakala.
“Kama itafika wakati nitafanya hivyo ina maana majukumu yangu ya kujihusisha na uongozi wa klabu unatakiwa usiwepo kwa sababu tayari kuna mgongano wa kimaslahi,” amesema Walter.
Amesema kama itatokea kujihusisha na masuala hayo itakuwa njia pekee ya kubaki kwenye tasnia ya mpira wa miguu, na kama uwepo katika upande huo maana yake kuna vitu anatakiwa kuacha ili kuepuka mgongano huo.
“Mimi nasimama kwenye majukumu yangu kama meneja wa timu ya Young Africans hakuna kitu kingine chochote cha ziada ambacho nakifanya,” ameongeza.
No comments:
Post a Comment