WAFANYABIASHARA WA MPUNGA KAGONGWA WALALAMIKIA UBOVU WA BARABARA KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 7 May 2024

WAFANYABIASHARA WA MPUNGA KAGONGWA WALALAMIKIA UBOVU WA BARABARA KAHAMA




Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Kahama  akizungumza na Huheso fm & Huheso fm

Wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda vidogo na kati vya kuchakata mpunga katika mji mdogo Kagongwa Wilaya ya Kahama Mkoa wa shinyanga wameiomba serikali kuwatatulia changamoto zinazowakabiri kama vile ubovu wa miundo mbinu ya barabara.

Kaimu meneja wa TARURA Kahama akizungumza na Huheso fm & Huheso fm

Na Neema Nkumbi huheso fm & huheso digital -Kahama

Wakizungumza na HUHESO DIGITAL wafanyabiashara hao wameeleza kuwa licha ya mapato makubwa yanayokusanywa na Halmashauri katika eneo hilo, bado wanashangaa kuona miundombinu yao ikiwa katika hali isiyoridhisha huku baadhi ya wafanyabiashara wakifunga vibanda vyao kutokana na magari ya mizigo kushindwa kuwafikishia mizigo katika maeneo yao.


"Miundo mbinu ya barabara ni mibovu sana kiasi ambacho tunapata tabu sana kuingiza mizigo huku viwandani hali inayopelekea kuanza kulipa hela tena kwa vijana wa mkokoteni kuingiza mizigo hivyo inatusababishia kupata hasara", amesema Alfonce Hungwi.


Pia mmliki mwingine Dauson Maganyiro amesema kutokana na ubovu wa barabara magari ya mizigo yanaharibika na kusababisha msongamano pia mizigo kushindwa kufika kwa wakati viwandani.


Naye Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa mchele Kagongwa ameeleza kuwa anazitambia changamoto na amewahi kutoa malalamiko hayo kwa baadhi ya vyombo vya habari na serikali kwa ujumla hivyo anaiomba serikali kulitazama eneo hilo kwa jicho la tatu kwani ni chanzo Cha mapato.


Kwa upande wake Eng Masola Juma kaimu meneja wa TARURA Wilaya ya Kahama amekiri kwamba eneo hilo Lina changamoto ya barabara ila tayari mkandarasi ameshapatikana na ameshasaini mkataba anasubiri mvua zikate aanze kazi.


"Nakiri kwamba changamoto hiyo ipo Kagongwa, mwaka Jana tulitengeneza barabara na mwaka huu tayari tumempata mkandarasi na ameshasaini mkataba hivyo mvua ikiisha tu ataanza kazi", amesema Eng Masola.


Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Robert Kwela amesema mwaka ujao wa fedha wametenga kiasi Cha shilingi bilion Moja na milion mia mbili Kwa ajili ya matengenezo ya miundo mbinu ya barabara kwa ujumla.






No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso