Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof Mohamed Janabi amesema kuwa wana mkakati maalum wa kutoa huduma za kisasa za matibabu kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kutoka visiwa vya Comoro kutokana na ongezeko la idadi yao katika siku za hivi karibuni.
Prof Janabi ambaye pia ndio Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa
ya Utalii wa Matibabu ameeleza kuwa kwa hivi sasa wana mratibu maalum wa
wagonjwa toka nje ya nchi na pia mkalimani wa lugha ya kifaransa ili
kurahisisha mapokezi ya wagonjwa toka Comoro na wako tayari kuwa na kliniki za
ufuatiliaji kwenye visiwa hivyo.
“Kwa idadi yao na inavyoongezeka,tunakusudia tuwe na wodi maalum ya wagonjwa wanaotoka Comoro katika siku za hivi karibuni” amesema Prof Janabi.
No comments:
Post a Comment