Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemtangaza Mgombea wa Nafasi ya Mkurugenzi wa Afrika katika Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Faustine Ndugulile ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bunge la Tanzania wa Jimbo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba (Mb.)
Akitambulisha sifa na uwezo binafsi wa mgombea huyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba (Mb.) amesema kuwa Ngugulile ni mgombea sahihi mwenye uwezo wa kazi na kufanya mageuzi na maboresho katika ya Sekta ya Afya.
Aidha,
ameeleza kuwa Ndugulile alipokuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Afya aliweka
kipaumbele cha kusimamia suala la kutunga, kusimamia sera na kuratibu mipango
mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha usimamizi wa sekta ya afya
nchini unaimarika kwa ajili ya kujenga nguvu kazi imara ya Taifa.
“Kupatikana
kwa nafasi hii kutaiwezesha Tanzania kuimarika zaidi katika utekelezaji wa
Diplomasia ya Afya ambayo ni muhimu katika Diplomasia yetu kwa ujumla hususan
katika usimamizi wa mipango, maarifa na rasilimali ulimwenguni.’’ Amesema Waziri Makamba
Mbali na hayo Waziri Makamba ameeleza kuwa kufauatia jitihada mbalimbali za kidiplomasia
zilizofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika
Mashariki tayari mgombea wa Tanzania ameungwa mkono na Nchi 16 Wanachama wa
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na nchi zingine 7 kutoka Afrika,
hivyo kuipa Tanzania mtaji wa jumla ya kula 23 katika kinyang’anyiro cha
kuwania nafaisi hiyo.
Naye Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemwelezea mgombea
Dkt. Ndugulile kuwa akiwa Naibu
Waziri katika Wizara ya Afya alifanya jitihada katika kuimarisha afya ya msingi
kwa kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kutoka Serikalini na wadau wa
maendeleo.
Waziri Ummy Ameongeza
kuwa Ndugulile ametoa mchango mkubwa kwenye usimamizi wa maboresho ya afya
ya mama na mtoto na lishe na chanjo ambapo usimamizi huo umewezesha kupunguza
kwa kiasi kikubwa vifo vya wajawazito na watoto.
No comments:
Post a Comment