SERIKALI YATOA MIEZI SABA KWA WAKALA WA MBEGU KUJENGA GHALA ZA KUCHATAKA MBEGU. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 20 May 2024

SERIKALI YATOA MIEZI SABA KWA WAKALA WA MBEGU KUJENGA GHALA ZA KUCHATAKA MBEGU.




Na Lucas Raphael,Tabora


Serikali imetoa miezi saba kwa wakala wa taifa wa mbegu za kilimo (asa) nchini kuharakisha mchakato wa ujenzi wa ghala la kisasa la kuhifadhia Mbegu zinazovunwa kwenye shamba la Mbegu Kilimo lililopo wilaya ya Nzega mkoani Tabora.


Mbegu hizo zaidi 500 zinazoendelea kuvunwa katika shamba hilo ambapo kwa sasa zimehifadhiwa katika eneo la muda la kuakaushia mbegu.


KAULI hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa kilimo David Silinde katika ziara ya kukagua maendeleo ya shamba hilo ambalo limeshawekewa miundombinu ya umwangiliaji ili liweze kuzalisha Mbegu bila kutegemea Mvua.


Alisema kwamba ili kulinda matokeo hayo mazuri itakapofika Mwezi Desemba 2024 ni lazima lipatikane ghala la kuhifadhi Mbegu hizo ili kuwahakikishia wakulima uhakika wa mbegu kama alivyo makusudio Mhe. Rais.


Akikagua Mbegu za mahindi zilizovunwa kwenye shamba hilo Naibu Waziri Silinde alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Dkt. Sami Suluhu Hassan alikuwa na lengo la kuiwezesha Nchi kujitosheleza kwa mbegu za mazao mbalimbali hivyo basi mavuno hayo ni matokeo ya maono ya Rais.


Aidha Silinde ameagiza kuanza kwa mchakato wa upatikanaji wa Mtambo wa kuchakata Mbegu ili kuepuka gharama za kusafirisha mbegu hizo kwenda kiwandani mjini Morogoro na baadae kurudishwa tena kwa wakulima.


"Mbegu zinazalishwa shambani Kilimi Nzega, kiwanda kipo Morogoro halafu itarudishwa Nzega na maoneo ya kanda ya Magharibi na Kanda ya ziwa itawaongezea gharama wakulima" Alisisitiza Silinde.


Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo Dkt. Sophia Kashenge alisema amepokea maelekezo hayo na atayatekeleza kama alivyoelekezwa.



Alisema Shamba la Mbegu Kilimi limeongeza Uzalishaji baada ya kufungwa Miundombinu ya Umwagiliaji hivyo uhitaji mkubwa wa ghala unahitajika kutoka na Mazao kuwa mengi shambani.



Alisema maelekezo hayo yote yatafanyiwa kazi kama inavyotakiwa ilikuepusha gharama zinazojitokeza wakati wa kusafirisha Mbegu hizo Morogoro kwenye Mtambo wa uchakataji.


Aidha Dkt, Sophia Kashenge aliipongeza wizara ya kilimo Kwa kuendelea kutoa ushiriano mkubwa kwa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA hasa katika kuhakikisha Uzalishaji wa Mbegu unaongezeka mara dufu.




Dkt, Sophia alisema Kwa msimu huu wa kilimo Wakala umeanza rasm kilimo Cha Umwagiliaji katika Shamba la Mbegu Kilimi kwa kulima Mahindi Hekta 150 sawa na Ekari 675.



Shamba la Kilimi lina ukubwa wa hekta 1100 ambapo eneo linalotumika kwa kilimo ni Hekta 802.5.




Kwa sasa shamba hilo limezalisha mbegu za mahindi hekta 250 za mtama, hekta 40 za alizeti pamoja na hekta 10 za choroko.



Naibu Waziri wa kilimo David Silinde akipokea maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo Dkt. Sophia Kashenge juu ya mtama usio shambuliwa na ndege unaolimwa katika shamba la kilimi wilayani nzega mkoani Tabora




Mahindi yaliyovunwa kutoka shambani yakiwa yameifadhiwa kwenye eneo hilo



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso