NA NEEMA NKUMBI - DAR ES SALAAM
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema serikali anatambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na vyombo vya habari vya mitandaoni pamoja na mchango wao katika maendeleo ya taifa.
Waziri Waziri Mkuu mesema hayo leo Mei 21, 2024 katika ukumbi wa Maktaba wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambapo amekuwa mgeni rasmi katika kongamano la Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA).
Waziri mkuu ameeleza kuwa katika miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Madarakani amewezesha kukua kwa sekta ya habari na ongezeko la vyombo vya habari na wasomaji wa habari mitandaoni.
Kufuatia mchango mkubwa wa wa vyombo vya habari mitandaoni, ameahidi serikali itashirikiana na wadau wa habari mitandaoni kupitia JUMIKITA pamoja na vyombo vingine ili kuhakikisha sekta hii inakua kwa maendeleo ya nchi.
Aidha ameitaka Wizara ya habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari, TCRA pamoja na wadau wengine wa habari kuandaa semina na mafunzo kwa Waandishi wa habari wa mitandaoni ili kuwajengea uelewa kuhusu Sheria kanuni na maadili ya fani ya habari.
Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknlojia ya habari,Nape Nnauye amesema watakaa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzanja (TCRA) kufanya Mapitio ya Sheria na kanuni ambazo zilikazwa sana ili zilegezwe, pamoja na mapitio ya Kodi na Tozo za kusajili blog na Online TV.
Mwenyekiti wa JUMIKITA Shaaban Matwebe,ameeleza kuwa baadhi ya viongozi wenye Mamlaka wamekuwa hawawathamini na Waandishi wa habari za Mitandaoni hasa wanapokuwa wakipiga Simu ili kuweka usawa katika habari.
Pia, ameziomba Mamlaka mbalimbali za Serikali kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa Mitandaoni Kitaaluma, ili kuepuka makosa yanayojitokeza.
Waziri wa habari, Mawasiliano na Teknlojia ya habari,Nape Nnauye akizungumza na Waandishi wa habari wa mitandaoni
No comments:
Post a Comment