RC SIMIYU AWAONGOZA WATUMISHI ZOEZI LA UPANDAJI MITI JENGO JIPYA LA UTAWALA NYAUMATA. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 27 May 2024

RC SIMIYU AWAONGOZA WATUMISHI ZOEZI LA UPANDAJI MITI JENGO JIPYA LA UTAWALA NYAUMATA.




Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt.Yahaya Esmail Nawanda amewaongoza Watumishi wa Taasisi mbalimbali katika zoezi la upandaji wa Miti katika Jengo jipya la Utawala lililopo katika Mji wa Kiserikali Nyaumata Mkoani humo.


Miti 150 imepandwa katika zoezi hilo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Kampeni ya "Mti wa Mama "iliyoasisiwa na Shirika la utangazaji Tanzania TBC ambapo kila Mwezi Tarehe 27, ni siku ya upandaji wa Miti Nchini ikiwa ni hatua ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi.


Mhe.Dkt.Nawanda ametoa wito kwa Watumishi Mkoani humo kuitunza miti hiyo ili kufikiwa malengo yaliyokusudiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso