MWANAUME AFARIKI AKIDAIWA KUNYWA POMBE KALI AINA YA GONGO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 27 May 2024

MWANAUME AFARIKI AKIDAIWA KUNYWA POMBE KALI AINA YA GONGO



Na Mapuli Kitina Misalaba

Mwanaume mmoja anayeitwa Manota Jidairifa mwenye umri wa Miaka 42 mkazi wa mtaa wa Tambukareli Manispaa ya Shinyanga amefariki Dunia kwa kile kinachotajwa kuwa baada ya kunywa pombe kali aina ya Gongo kupita kiasi.

Tukio hilo limetolea leo mchana Mei 27,2024 baada ya mwanaume huyo kukutwa amefariki katika eneo la relini mtaa wa Tambukareli kata ya Ndembezi Mkoani Shinyanga.

Agnes Jidairifa ambaye ni dada yake na marehemu ameeleza kuwa Manota amefililiza wiki moja akinywa pombe ya kienyeji aina ya Gongo na kwamba alikuwa anakataa kula chakula nyumbani hali ambayo inatajwa kusababisha kifo chake.

“Yaani kaka yangu amekunywa Pombe kwa mfululizo wiki nzima kabisa nilijitahidi kumwambia kwanini unayanywa kwa fujo hivi na ukiyanywa mpaka unakuja nayo nyumbani ya nini, tukiivisha ukimtengea chakula anafinya kidogo tu anaacha ile juzi alikuja muda wa saa tisa nikamuuliza umekula akasema hajala nikasonga ugali nikampa na penyewe akajaribu kidogo tu akauacha akaenda kuyafuata tena mapombe akarudi amelewa nikamwambia kula sasa akasema nitakula tu”.

“Jana pia aliamka asubuhi akaenda vizuri muda wa saa tisa akarudi tena yaani alirudi hata sauti yake iko mbali ugali kwa kweli hakuuweza ndo tukakoroga uji, leo tena asubuhi tumekoroga uje umeshaiva sasa amenawa tu akatoka akaenda tena nikamwambia kaa unywe uje kwanza ndo uende unakoenda akasema mnanichelewesha sasa tumekaa muda ndiyo tumekuja kuitwa na watu kwamba twende huku kumbe ameyanywa mapombe wakati anarudi alipofika relini kabla hajavuka akawa amekaa hapo kwenye jua nafikiria namapombe ndo yakazidi kumaliza ngumu mwili, mimi nilipoijiwa nikakuta hali kama hiyo sasa”.amesema Agnes

Baadhi ya majirani katika familia hiyo ya marehemu wameiomba serikali kuchukua hatua kali kwa watu wanaouza pombe haramu huku wakiwasisitiza hasa vijana kuacha kutumia pombe hiyo.

Wananchi hao wamesema matukio ya namna hiyo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara ambapo wamesisitiza serikali kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaofanya biashara ya pombe bila kibali.

Misalaba Media imezungumza na kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi amekili kupokea taarifa za tukio hilo ambapo amesema jeshi la Polisi linaendelea kufanya misako ili kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaouza pombe haramu.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga majira ya saa saba mchana leo Mei 27,2024 tulipokea taarifa kutoka kwa wananchi kwamba maeneo ya mtaa wa Tambukareli kata ya Ndembezi tarafa ya mjini ndani ya Wilaya na Mkoa wa Shinyanga alikutwa mtu mwenye jinsia ya kiume akiwa amefariki ambaye amejulikana kwa jina Manota Jidailifa kwamba alikutwa akiwa amefariki na inasadikika ni baada ya kunywa pombe kali kupita kiasi jeshi la Polisi baada ya kupata taarifa tumefika kwenye eneo la tukio na tayari mwili umechukuliwa na kupelewa Hospitali baada ya hapo mwili utakabidhiwa ndugu kwa ajili ya mazishi”.

“Sisi bado tunaendelea na suala la uelimishaji na ndiyo maana hawa polisi kata walioko kwenye kata wanafanya mikutano na wananchi pamoja na mimi mwenyewe kamanda wa Mkoa tunawapa elimu wananchi suala la pombe kali pombe aina ya gongo ni pombe ambayo ni haribifu lakini pia inazoofisha afya na sisi tunaendelea kufanya misako na doria kuhakikisha kwanza hili suala linakaa sawa”

“Lakini suala linguine sasa tunakuja kwa hao vijana ni malezi kwahiyo wazazi, sisi jeshi la polisi, ustawi wa jamii na taasisi mbalimbali sote kwa pamoja tuhakikishe kwamba suala la malezi tunalisimamia kuanzia ngazi ya familia kwahiyo viongozi wa dini na wananchi tutoke kwa pamoja tukiwa kama wazazi au walezi kuhakikisha kwamba kizazi hiki cha hawa vijana ambao wameibukia kwenye matendo ya hovyo hovyo tunakemea sote kwa nguvu moja”.amesema SACP Magomi

Agnes Jidailifa ambaye ni dada yake na marehemu 


Baadhi ya majirani wakiwa katika familia ya marehemu.

Eneo ambalo marehemu amekutwa akiwa amefariki.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso