Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 2 hadi miaka 2.5, anadaiwa kulawitiwa na kijana mwenye umri kati ya miaka 15-16 mkazi wa mtaa wa Nyasubi kata ya Nyasubi manispaa ya Kahama wakati akiwa nacheza nje ya nyumba yao.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo Susana Richard na Happy Daud, wameeleza namna tukio hilo lilivyotokea na kulaani kitendo cha kijana aliyemuokota mtoto huyo kushikiliwa kama mtuhumiwa.
"mimi ni jirani wa huyu mama nilisikia akipiga kelele nilipoenda nikamuliza mtoto ulikuwa wapi akaeleza alikuwa chumba jirani akamtaja hadi jina", amesema Susana Richard .
"haiwekani mtu unamsaidia halafu unasingiziwa kwa ni wewe umefanya tukio hali hii inatusababishia kushindwa kutoa msaada inapotokea tatizo kwa kuhofia kukamatwa" amesema Happy Daud.
Makamu mwenyekiti wa SMAUJATA wilaya ya Kahama Juma Mpei aliyefika katika eneo la tukio ameeleza hatua za awali zilizochukuliwa.
"tumepokea taarifa kwa kuna mtoto amelawitiwa na mama amebaini baada ya kukuta njia ya haja kubwa kuna uchafu na damu na hatua za awali tulizochukua tumewakamata watuhumiwa na tunawapeleka polisi" amesema Juma Mpei
Mwenyekiti wa mtaa huo Leonard Mayala alikiri kutokea kwa tukio hilo kwenye mtaa wake na kuwataka wazazi au walezi kuwa makini na Watoto wao.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Kenedy Mgani akizungumza kwa njia ya simu ameeleza kuwa bado halijafika mezani kwake, analifuatilia na kuahidi kulitolea taarifa kamili baadae.
No comments:
Post a Comment