Na Anas Ibrahim-Huheso Fm
Imeelezwa kuwa Sofia Budeba mkazi wa kijiji cha Nyangota katika Kata ya Ngaya Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga, Sofia Budeba anadaiwa kujifungua mtoto amevunjika mkono.
Akizungumza na wanahabari Sofia Budeba amesema alifika katika Zahanati ya Ngaya hapo siku ya Jumamosi ambapo kabla hajajifungua aliombwa fedha na wauguzi kiasi cha shilingi Elfu arobaini kwa ajili ya dawa ya kuongeza kasi ya uchungu.
Akielezea tukio hilo mume wa Sofia Budeba, ambaye ni Jumanne Mkabile amesema mke wake alijifungua salama lakini mara baada ya kubainika mtoto amevunjika mkono wahudumu walimuomba kiasi cha shilingi laki moja na Elfu Hamsini kwa ajili ya kumhudumia mtoto.
Mkabile amesema aliwapatia kiasi hicho cha fedha na suala hilo alilifikisha kwa diwani wa Kata ya Ngaya ambapo watoa huduma walirejesha fedha hizo
Philip Laizer ni msimamizi wa kitengo cha watoto wachanga katika hospitali ya Manispaa ya Kahama, amekiri kumpokea mtoto huyo akiwa amevunjika mkono.
Aidha baada ya tukio hilo kutokea mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha amefika katika hospitali ya Manispaa ya Kahama alipolazwa mtoto huyo baada ya kuhamishwa kutoka kituo cha afya Ngaya huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba wanasiasa kuacha kutumia matukio kwa maslahi ya kisiasa.
No comments:
Post a Comment