Wanafunzi watatu (3) wa shule ya sekondari John Paul wa pili Iliyopo Mtaa wa Mbulu Kata ya Mhongolo Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wamefariki dunia kwa kukosa hewa baada ya kuingia kwenye kihenge cha kuhifadhia mahindi kwa lengo la kutoa mahindi hayo kwa ajili ya chakula Jambo ambalo limepelekea kifo chao.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza wakati wa kuaga miili ya wanafunzi watatu waliofariki dunia kwa kukosa hewa safi kwenye kihenge cha mahindi
NA NEEMA NKUMBI HUHESO DIGITAL& HUHESO FM
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha ameyasema hayo kwenye ibaada ya kuaga miili ya Wanafunzi hao iliyofanyika kwenye viwanja vya Jimbo Katoliki la Kahama Mjini Wilayani Kahama.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa vijana watatu wanaosoma kidato cha tatu katika shule ya Sekondari John Paul wa pili walikuwa wameingi kwenye Kihenge cha kutolea mahindi kwaajili ya chakula na hawakujua madhara ya Kihenge hicho na hewa haitoshi hali ambayo ilisababisha kifo chao.
Akitoa salamu za Rambirambi kwa Wafiwa, mdhibiti wa Ubora wa Elimu wa kanda Edith Mwijage Amesema kuwa amesikishwa na tukio la vijana hao na kutumia nafasi hiyo kuwaomba wazazi kuwa na subira wakati wakati wa kipindi hiki kigumu ambapo wamepoteza wapendwa wao.
Naye Japhet Daud Mdadila akizungumza kwa niaba ya wazazi wenzake amesema kuwa kwao kama wazazi pamoja na kanisa na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla huo ni msiba mzito na wameupokea kwa masikitiko makubwa.
"Sisi wanadamu tumezaliwa na mwanamke siku zetu zinahesabika, Viongozi wa Dini wametuhubilia hata tungelaumu kiasi gani na hata tungesema changamoto nyingi sana nasi hili tumepewa ni somo kwetu.
Pia amesema kuwa anafurahi kuona wazazi wamepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa mamlaka za serikali na hata shule yenyewe na kubainsha kuwa tukio lililotokea linatafakarisha katika mafunzo.
Askofu wa Jimbo Katoliki la Kahama ........amesema kuwa anaamini kadili walivyoishi mema yao nasi tukiendelea kuwaombea watasamehewa mapungufu waliyokuwa nayo kwa sala zetu na maombezi yetu na bado wakaendelea kufurahia maisha huko pamoja na Mungu.
Waliofari kwa ajari hiyo ni pamoja na Jonathan Daud Mdadila (17) Mkazi wa Nzega, Ibrahim Juma Said (17) Mkazi wa Mwanza pamoja na Paul Emmanuel John (18) Mkazi wa Kahama.
Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Kenedy Mgani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa, Tukio hilo lilitokea May mosi mwaka huu, majira kati ya saa tano na saa sita mchana shuleni hapo, na kwamba walifariki dunia kwa kukosa hewa safi baada ya kuingia kwenye kihenge cha kuhifadhia Mahindi.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe Amina.
No comments:
Post a Comment