Tanzania haitamsahau Dikteta Idd Amini Dada aliyeitawala Uganda kwa mabavu kisha kuvamia Tanzania mwaka 1978 ambapo Tanzania iliingia vitani na kufanikiwa kumng'oa mvamizi huyo mwaka 1979.
Luteni Kanali
Mstaafu Daniel Gangisa wakati wa uhai wake akiwa na rafiki yake Dikteta Idd Amini
Dada aliyeitawala Uganda kwa mabavu kisha kuivamia Tanzania mwaka 1978 ambaye
aling’olewa na majeshi ya Tanzania mwaka 1979
Luteni Kanali Mstaafu Daniel Gangisa pichani kulia akiwa na rafiki yake
Dikteta Idd Amini Dada amefariki Dunia Mei 6,2024 nyumbani kwake Chandarua
Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,ratiba ya maziko itatolewa na ndugu wa
marehemu .
Akihojiwa na mwandishi wa Makala haya wakati wa uhai wake Luteni kanali
Mstaafu Gangisa anasema anamfahamu vizuri Dikteta Idd Ami kwa sababu walisoma
na kufanyakazi pamoja kwa miaka mitatu Nakuru nchini Kenya.
Gangisa alizaliwa mwaka 1927
katika eneo la Ruhuwiko mjini Songea ambapo alijiunga na jeshi la wakoloni
mwaka 1947 ambapo mwaka 1953 alikwenda chuo cha Jeshi Nakuru Nchini Kenya ili
kupata mafunzo Zaidi ya kijeshi ambako alikutana na Dikteta Idi Amini.
“Nimesoma
na Idd Amini miaka mitatu kuanzia 1953 hadi 1955 alikuwa rafiki yangu
sana,tulikuwa tunalala chumba kimoja bwenini, baada ya kumaliza kozi mimi na
Amini tulipata alama za juu hivyo chuo kilitupa mkataba wa kuwa walimu
tulifanya kazi sote tukiwa na cheo cha Sajenti kwa miaka mitatu,” alisema Luteni Kanali Mstaafu Gangisa enzi za uhai wake
Hata hivyo Gangisa anasema licha ya Amini katika kipindi hicho kuonekana
kuwa ni kijana mtulivu na ambaye hakuwa mgomvi sana isipokuwa alikuwa mpiganaji
wa ngumi na kwamba Amin alimwomba Gangisa amfundishe ngumi,lakini alikataa.
Gangisa anasema kwa muda alioishi na Idd Amin aligundua dosari kubwa
aliyokuwa nayo tangu kipindi hicho Dikteta Idd Amin alipenda sana vyeo hata
aliposikia amepindua nchi hakushangaa kwa sababu alimfahamu.
Luteni Kanali Mstaafu Gangisa anasema baada ya kumaliza mkataba wa
kufundisha Nakuru alirudi Nyeri nchini Kenya kambi yake ya Jeshi kuendelea na
Vita ya Maumau kisha alikwenda kwenye vita nchini Mauritius na Idd Amin alirudi
kwao Uganda ambapo mara ya mwisho kuonana na Idd Amin anasema ilikuwa mwaka
1960 nchini Kenya.
Anasema mwaka 1964 alishiriki katika kuunda JWTZ Jeshi jipya lenye
heshima nchini Tanzania na kwamba yeye ni miongoni mwa maafisa waliunda JWTZ
ambapo yeye ni Ofisa wa 50 wakati huo akiwa na cheo cha Luteni Kanali.
Kwa mujibu wa Luteni Kanali Mstaafu huyo,Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius
Nyerere wakati anaanza harakati za uhuru na kuunda chama cha TANU yeye alikuwa
na Idd Amini Nakuru Kenya.
Idd Amini ndiye aliyenipa taarifa kwamba wewe Mswahili nyumbani kwako
kuna bwana ameanzisha Chama cha kupigania uhuru,alinitisha kwamba MAUMAU
itaamia kwetu,nikamwambia Mungu yupo,alikuwa anaongea Kiswahili kizuri,alikuwa
rafiki yangu mkubwa sana,alisisitiza Gangisa.
Gangisa aliacha kazi ya JWTZ mwaka 1978,lakini baada ya kusikia Idd Amini
amepindua nchi ya Uganda na kuvamia sehemu ya Kaskazini ya Tanzania aliamua
kurudi jeshini kupambana na rafiki yake Idd Amin.
“Nilisema
kama amevamia nchi yetu narudi jeshini, tulipambana naye, nilifika hadi
kijijini kwake ,Kampala pale alinusurika kuuawa, akatorokea njia ya Kenya, tuliwaomba
Kenya wafunge mpaka walikataa hivyo Idd Amin akanusurika akatoroka ukawa ndiyo
mwisho wa Vita ya Uganda ” alisema Luteni Kanali Mstaafu Gangisa enzi za
uhai wake.
Luteni Kanali Mstaafu Gangisa pia anasema alishirikiana na Samora Machel
wa Msumbiji wakati wa harakati za kupigania Uhuru wa Msumbiji ambapo mara
kadhaa amelala kwenye mashimo na Samora Machel.
Anasema Samora Machel mara baada ya Uhuru alifika Songea mwaka 1975
wakati anazungumza na wananchi alimshukuru Luteni Kanali Gangisa akisema
alishiriki naye kwa kutoa silaha na walilala wote kwenye mashimo na kula mihogo
ya watu wakati wa mapambano ya wareno.
Gangisa anatoa rai kwa serikali kuwakumbuka wastaafu waliolitumikia Taifa
kwa uzalendo mkubwa ili kumalizia kwa furaha maisha yaliobaki hapa duniani.
Chanzo : FullShangwe
No comments:
Post a Comment